
Wakati serikali ikipiga marufuku disko
la mitaani maarufu kwa jina la ‘Vigodoro’ bado kuna baadhi ya mikoa
inapuuza agizo hilo ambapo mwanamke mmoja ambaye mumewe anafanya kazi
kwenye mgahawa uliopo ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani
Morogoro, aliyetajwa kwa jina la Mama Abdul (pichani), amejitoa fahamu
kupitia Kigodoro na kujikuta akisaula nguo hadharani.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na mwanahabari wetu lilijiri juzikati, majira ya mchana kwenye kigodoro mbele ya watoto waliopokea ekaristi takatifu katika Kanisa la Mtakatifu Monica lililopo maeneo ya Kihonda mkoani hapa.
Mke huyo wa mtu alimwaga ‘lazi’ hizo kwa kushirikiana na mdogo wake wa damu aliyefahamika kwa jina moja la Jacqueline wakati wakimpongeza mtoto wa rafiki yao aliyepokea ekaristi.

No comments:
Post a Comment